Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) (Tanzania People's Defense Force TPDF) ni jeshi lililoanzishwa mnamo mwezi wa SEPTEMBA mwaka wa 1964. Ilichukua nafasi ya jeshi la
Tanganyika Rifles lililorithiwa na ukoloni wa Kiingereza.
Historia ya awali
Chanzo cha jeshi nchini Tanzania kilikuwa
jeshi la kikoloni la Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Mwaka 1919 Uingereza
ilikabidhiwa utawala juu ya TANGANYIKA na SHIRIKISHO LA KIMATAIFA. Waingereza
walipanusha mfumo waKING’S AFRICAN RIFLES waliowahi
kuanzishwa KENYA hadi Tanganyika.
Jeshi la Kings African Rifles ilikuwa na vikosi (battalions) 6 ambazo viwili
vilikuwepo Kenya, vitatu Tanganyika na kimoja huko Uganda. Katika kikosi cha
sita cha King's African Rifles kilichoanzishwa mwaka 1917 kwa kuajiri askari
kutoka Tanganyika walikuwepo pia askari wa awali wa jeshi la Kijerumani la SCHUTZTRUPPE waliowahi kukamatwa kama
wafungwa na kukubali kuendelea upande wa Waingereza.
Baada ya uhuru mwaka 1961 vikosi vya Kings
African Rifles katika Tanganyika vilibadilishwa jina na kuwa Tangayika Rifles
(TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na
Kings African Rifles (KAR). Maafisa wenye mamlaka bado walikuwa Waingereza,
pamoja na Waafrika watano waliopandishwa cheo wakati wa uhuru na kupokea
mafunzo katika vyuo vya kijeshi vya Kiingereza. Jeshi jipya lilipangwa katika
vikosi viwili vyenye makao makuu huko DAR
ES SALAAM na TABORA. Afisa mkuu alikuwa Brigedia
Jenerali Patrick Sholto Douglas.
Mgomo na uasi wa
Tanganyika Rifles
Kwa jumla kulikuwa na hali ya kutoridhika
kati ya askari wa TR. Sababu yake ilikuwa matumaini ya kwamba uhuru ungeleta
mabadiliko makubwa zaidi na nafasi za kupanda cheo baada ya kuondoka kwa
maafisa wazungu. Lakini maafisa Waingereza waliendelea kuajiriwa na serikali ya
Nyerere na tofauti kubwa katika mapato na hali ya makazi ya Wazungu na Waafrika
ziliendelea. Hata kinyume askari waliowahi kuwa na mshahara wa juu kulingana na
watumishi Waafrika wengine ya serikali waliona ya kwamba mapato yao hayakupanda
ilhali mishahara kwa jumla iliongezeka zaidi. Zaidi ya hapo, serikali ya TANU ilituma vijana kutoka Umoja wa
Vijana wa TANU kwa mafunzo ya kijeshi huko ISRAEL
na baada ya kurudi walipewa ajira jeshini na wengine wao kupandishwa vyeo
kupitia askari waliowahi kuhudumia miaka mingi.
Katika Januari 1964 matokeo mawili
yalijadiliwa sana kati ya askari moja ilikuwa tangazo la Nyerere alikotamka
mwisho wa siasa ya "Africanization" katika utumishi wa serikali[2]. Tangazo hili lilisababisha viongozi wa
umoja wa wafanyakazi kulalamika. Tukio lingine likawa habari za MAPINDUZI YA ZANZIBAR yaliyoanza tar. 12 Januari 1964.
Tarehe 20 Januari 1964, bado wakati wa
usiku, kikosi cha kwanza cha TR kwenye kambi la Colito Barracks mjini Dar es
Salaam kiliasi na kujipatia silaha kutoka ghala. Maafisa Waingereza walikamatwa
na kufungwa lakini mkuu Douglas aliweza kujificha. Waasi walivamia kituo cha
redio, uwanja wa ndege, ikulu na ofisi ya posta na simu. Maafisa Waingereza na
Waafrika wasioshiriki na waasi walisafirishwa Kenya. Rais Nyerere alienda
mafichoni katika kanisa moja la kikatoliki ng'ambo ya bandari akamwachia waziri OSCAR KAMBONA kazi ya kuwasiliana na wanajeshi.
Madai ya wanajeshi yalikuwa kuachishwa kwa maafisa Waingereza na kupandishwa
kwa mishahara. Siku za kwanza ya mgomo wa jeshi ilifuatwa na vipindi vya fujo
mjini vilivyobadilika na vipindi vya kimya, mashambulizi dhidi ya maduka ya
Wahindi na kukamatwa kwa Wazungu wachache. Hata mbalozi wa Uingereza alikamatwa
kwa kipindi kifupi.
Waziri Kambona alianza kujadiliana na wanajeshi
na kuwaahidi ongezeko la mapato na kutoa vyeo vya juu kwa Waafrika kadhaa.
Nyerere alirekodi hotuba iliyotangazwa redioni alipokosoa wanajeshi na kudai
utulivu. Askari walirudi kwenye kambi lakini kurudi mjini siku iliyofuata. Pia
huko Nairobi na Kampala ulitokea uasi wa wanajeshi -wote askari wa KAR wa
awali. Maraisi Milton Obote na Jomo Kenyatta hawakusita kuomba vikosi wa jeshi
la Uingereza vilivyokuwa bado na vituo kwa kuzimisha ghasia. Hatimaye Nyerere
alianza mawasiliano na Uingereza iliyotuma manowari na wanajeshi kutoka Aden
kuelekea Dar es salaam.Polisi ya siri ya Tanzania ilianza kupata habari ya
kwamba pia kati ya askari ya Field Force unit majadiliano yalikuwa yameanza
kuunga mkono na juhudi za wanajeshi, pia harakati kati ya wafanyakazi bandarini
na hofu ilikuwa ya kwamba sehemu ya viongozi wa umoja wa wafanyakazi walikuwa
na mipango ya kujiunga nao.
Tarehe 24 Januari serikali ya Tanzania
iliomba rasmi Uingereza kuingia kati na kuzimisha uasi. Asubuhi ya 25 Januari
kikosi kidogo cha wanajeshi wa Kiingereza waliondoka kwenye meli iliyokwepo
karibu na Dar es Salaam kwa njia ya helikopta. Walivamia kambi la Colito
barracks na jenerali Douglas alidai kwa kipazia sauti wanajeshi wajisalimishe.
Mwanzoni walikataa lakini baada ya mashambulio mafupi walio wengi
walijisalimisha wengine wakakimbia. Viongozi walikamatwa, na pia askari wa
Dodoma na Nachingwea waliowahi kujiunga na uasi walijisalimisha bila upinzani
kwa askari Waingereza wachache.
Wakazi wengine wa Daressalaam walikuwa na
hofu ya kwamba Uingereza ulikuwa umerudi ili kurudisha ukoloni lakini baada ya
kusita masaa machache Nyerere alieleza kwa njia ya redio ya kwamba kuingilia
kwa Uingereza ulifuata ombi la serikali yake.
Watu wengi walikamatwa baada ya matukio
haya na kufanyiwa utafiti kama walikuwa na uhusiano na uasi.
Askari Waingereza waliondoka kwenye Aprili
1964 na nafasi yao ilichukuliwa na kikosi kutoka NIGERIA iliyofika kwa niaba ya UMOJA WA AFRIKA kufuatana na ombi la serikali ya
Tanganyika.
Kuanzisha jeshi jipya
Baada ya uasi, jeshi la TR lilivunjwa.
Askari wote waliachishwa. Sehemu ya askari wa Dodoma waliajiriwa tena katika
jeshi jipya lakini hao wa Dar es Salaam hawakurudishwa. Maafisa Waafrika ambao
kwa jumla walisimama upande wa serikali na kutoshiriki katika uasi waliajiriwa
tena.
Jeshi jipya lilijengwa kwa kuajiri hasa
wanachama wa umoja wa vijana wa TANU.
Jeshi hili jipya liliwekwa chini ya usimamizi ya chama cha TANU (baadaye CCM)
kwa kufuata mtindo wa nchi kama Urusi na China. Kamanda wa kwanza alikuwa MRISHO SARAKIKYA aliyewahi kusimama upande
wa serikali wakati wa uasi akapandishwa cheo kutoka luteni hadi kanali, baadaye
kuwa jenerali.
Mwanzoni JWTZ ilikuwa jeshi ndogo lenye
askari chache kuliko TR lakini hadi 1967 lilipanushwa kuwa na vikosi 4.
Mpangilio
wa JWTZ wa kisasa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limegagiwa kwa
matawi matatu:
·
Kamandi
ya Nchi Kavu
·
Kamandi
ya Jeshi la Majini
·
Kamandi
ya Jeshi la Anga.
Nchi Kavu
Mnamo mwaka 2012 Jeshi la Nchi Kavu la JWTZ
lina vikosi vifuatavyo:
·
5 ×
brigedi za askari wa miguu
·
1 ×
brigedi ya vifaru
·
3 ×
batalioni ya mizinga
·
2 ×
batalioni za mizinga ya ulinzi wa hewani
·
1 ×
batalioni ya mizinga ya mortar
·
2 ×
batalioni za kupambana na vifaru
·
1x
rejimenti ya uhandisi
·
1 ×
kundi la logistic na akiba
Wajibu wa JWTZ ni rasmi
·
Kulinda Katiba na
Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
·
Ulinzi wa mipaka ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
·
Kufanya mafunzo na
mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote.
·
Kufundisha umma
shughuli za ulinzi wa Taifa.
·
Kushirikiana na
mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa
·
Kutoa huduma
mbalimbali za kijamii.
·
Kukuza elimu ya kujitegemea
na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
·
Kushiriki ulinzi wa
amani kimataifa.
CHANZO:WIKIPEDIA
Post a Comment