5.KUJIKUNJA KWA NGOZI YA VIDOLE VYA MIKONO BAADA YA KULOWA AU KUKAA MUDA MREFU KWENYE MAJI.
Je umewahi shuhudia jinsi ngozi ya vidole vyako inavyojikunja baada ya kufua nguo muda mrefu au kushika maji muda mrefu? Unajua ni kwa sababu gani ngozi hujikunja kama ya mtu aliyezeeka angali yu kijana mara baada ya kukaa sana kwenye maji?
Watu wengi kabla
walizani kwamba kujikunja kwa ngozi hiyo hutokana na maji kuingia kwenye ngozi
na hivyo ngozi hujikunja baada ya kulowa.
Lakini wanasayansi
baada ya kufanya utafiti kwa muda merefu juu ya nini hasa hupelekea ngozi
kujikunja? Walisema HAPANA si kwa sababu ya ngozi kulowana. Na walikuja na
majibu haya.
Mwili unapokutana na
majimaji mara moja hupeleka taarifa na kutafsiri kwamba mazingira hayo yana
UTELEZI (Slippery) hivyo kutasababisha mikono kushindwa kushika (Grip) au
kukamata vitu kwa urahisi kutokana na utelezi huo. Hapo mwili huchukua hatua ya
haraka kuikunja ngozi ya mikono yako ili kurahisisha ushikaji wa vitu
vinavyoteleza ndani ya maji pamoja na kutembea kwenye utelezi.
6. VIPELE VIPELE VYA
BARIDI KWENYE NGOZI (GOOSEBUMPS)
Kazi kubwa ya vipele hivi ni kupunguza kiasi cha joto la mwili linalopotea kupitia matundu ya ngozi. Hivyo kwa kufanya hivi humfanya binadamu kutunza joto la mwili hata katika mazingira ambayo hali yake ya hewa si rafiki kwa mwili wa mwanadamu au ni yenye baridi sana.

7. MACHOZI (TEARS)
Zaidi ya kuwa majimaji (MUCOUS MEMBRANE ) yanayopatikana kwenye Macho ambayo kazi zake ni kulilinda jicho dhidi ya kitu chochote kigeni kinachoingia jichoni (mfano unapokata vitunguu au mdudu anapoingia jichoni huwa unatoa machozi mengi eeeh!! Pia dhidi ya upepo na moshi) na pia hutumika kama kilainishi cha jicho pale linapokuwa linazunguka zunguka (blink).

Vilevile machozi yana
kazi ya kupunguza HISIA ZA HUDHUNI zinazozalishwa mwilini. Wanasayansi
wanaamini kuwa mtu anapokua mwenye msongo wa mawazo (stress) mwili hutengeneza
kitu kipya ili kwenda kubugudhi na kuharibu maumivu yote ambayo mtu anajisikia.
Hivyo machozi yanayozalishwa hapa huwa na kemikali na yanafahamika kama NATURAL
PAINKILLER. Machozi haya ni tofauti na machozi ya kawaida, lengo lake hasa la
kuzalishwa ni kwa ajili ya kuondoa kabisa maumivu yaliyozalishwa mwilini
Hivyo mpaka hapa
tumeona kua kuna machozi ya aina tatu ambayo ni
i. Basal tears (vilainishi)
ii. Reflex tears (mlinzi)
iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)
i. Basal tears (vilainishi)
ii. Reflex tears (mlinzi)
iii. Emotion tears (mtuliza maumivu)
8. KUSHTUKA
USINGIZINI (MYOCLONIC JERKS or HYPNIC JERK).
Je! Ushawahi kutokewa na hali hii? umelala halafu ghafla unashtuka usingizini kwa mguvu nyingi kama umepigwa na shoti ya umeme na akili inakurudi ghafla huku mapigo ya moyo yakikuenda mbio? Na hali hii ikakutokea pasipo hata kuota ndoto yoyote?

Basi usiogope au
kuwasingizia watu uchawi, hii ni hali ya sayansi ya mwili.na ni njia moja wapo
katika ile mifumo ya mwili kujilinda.
Je hutokeaje?
Hii ni hali ya ajabu
sana isiyofanywa kwa hiari ambayo huwatokea watu mara tu wamejinyoosha
kitandani na kupitiwa na usingizi, mwili hutetemeshwa na kusukumwa kwa nguvu na
mtu hushtuka katika hali kama vile kapigwa na shoti ya umeme. Hali hii inaweza
kupelekea mtu hata kuanguka kitandani na humwamsha mara moja kutoka usingizini.
Wanasayansi
wanatuambia kua, pale tu unapopata usingizi kiwango cha upumuaji kinashuka
ghafla, mapigo ya moyo nayo taratibu yanapungua, misuli inatulia kwa ku-relax,
Kitu cha AJABU hapa ubongo unatafsiri hali hii kama ni DALILI ZA KIFO (brain's
misinterpretation of muscle relaxation), hivyo huchukua hatua za haraka za
kuushtua mwili kwa kuutetemesha au kuuskuma kwa nguvu, hali ambayo humfanya mtu
kuamka kutoka usingizini kwa KURUKA kitu ambacho ni hali isiyo ya kawaida.
Hali hii ikimtokea
mtu huambatana na kuongezeka kwa mapigo ya moyo (rapid heartbeat), kuhema
haraka haraka, na wakati mwingine mtu hutokwa na jasho jingi.
Wakati mwingine mtu
huamka ametoa macho na kama ukimwangalia, nae huishia hukuangalia tu huku
akikosa la kukujibu endapo utamuuliza vipi kuna tatizo gani?
MWILI WAKO NI ZAIDI
YA UNAVYOUJUA. JAMBO LA MSINGI NI KUONDOA HOFU KWANI MWILI WAKO UNAJUA NINI UFANYE
NA WAKATI GANI ILI KUKULINDA USIKU NA MCHANA KATIKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO.
Imeandikwa na;
Izengo Kadokado
November 2016.
Imeandikwa na;
Izengo Kadokado
November 2016.
Post a Comment