0

1. Ukiazima simu ya mtu uitumie, usianze kuangalia mambo yake kama vile kusoma message au kuangalia picha zake bila kuomba ruhusa.
2. Kama mtu akikupikia chakula, wewe msaidie kuosha vyombo baada ya kula.
3. Ukikuta "missed call" kwenye simu yako, mtumie message haraka mtu aliyekupigia kama huwezi kumpigia simu kwa wakati huo.
4. Hakikisha hausahau kurudisha kitabu ulichoazima.
5. Mtu akikununulia chakula au kinywaji hakikisha nawewe unamnunulia ndani ya wiki hiyo hiyo.
6. Ukiwaomba rafiki au ndugu zako waje wakusaidie kazi fulani nyumbani kwako, wapikie chakula kama malipo yao.
8. Usibishane kuhusu jambo fulani mbele ya watu wengi, tafuta sehemu nyingine ya kubishania ambayo watu hawatakerwa na sauti ya hoja zako.
9. Lipa deni lako haraka iwezekanavyo bila kujali deni hilo ni dogo kiasi gani. Ondoa fikra kwamba aliyekukopesha hazihitaji na lipa kabla hajakwambia anazihitaji.
10. Punguza sauti endapo unaangalia video au unacheza gemu katika simu yako sehemu yenye watu wengi, kama huwezi kupunguza sauti basi tumia Headphones.
11. Usivute Sigara kama mtu uliyekaribu nae hapendezwi na kitendo hicho, hata kama amekuruhusu uvute, lakini wewe kwa kumwangalia ukagundua hayuko comfortable.
12. Kama ukilala nyumbani au chumbani kwa mtu, hakikisha unatandika kitanda kabla ya kuondoka.
13. Usiweke LOUDSPEAKER kama mazungumzo yenu kwenye simu ni ya watu wawili tu, utaweka loudspeaker pale tu mikono yako haiwezi kushika simu.
14. Mara zote ukiwa unakula sahani moja na mtu aliyenunua chakula hicho achia kipande cha mwisho cha chakula kimaliziwe na mtu huyo. Labda kama aliyenunua chakula hicho kakataa kabisa kula.
15. Unapoazima Gari ya mtu kwa matumizi yako, jaza mafuta kama njia ya kusema Asante.
16. Usivunje mahusiano ya kimapenzi na mtu kupitia messages

Iimeandikwa na: IZENGO KADOKADO

Post a Comment

 
Top